BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KATIKA ukumbi wa mikutano wa Klabu ya Simba uliopo Makao Makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kumefanyika kikao cha ndani kati ya viongozi na wazee wa klabu, maalumu kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu klabu hiyo pamoja na suala la mfanyabiashara Mohamed Dewji 'Mo' kutaka kuinunua klabu hiyo.

Mzee Hassan Dalali aliyesimama, akizungumza katika kikao hicho

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Rais Evans Aveva kilisema wazee hao walioongozwa na wazee wa Baraza la wadhamini walijadili kwa pamoja na kukubaliana kuwa klabu hiyo ina uwezo wa kujiendesha na kwamba ofa ya Sh 20 bilioni iliyotolewa na Mo ni ndogo ukilinganisha na thamani halisi ya klabu hiyo. 

Wazee kutoka Baraza la Wadhamini waliokuwepo ni Mzee Mtika, Ramesh Patel, Hassan Dalali na Bi Hindu na kikao hicho kilimalizika kwa kauli moja ya 'kuipiga chini' ofa ya Mo na badala yake itangazwe tenda ili kutoa nafasi kwa wafanyabiashara mbalimbali ambao ni wanachama wa Simba, akiwemo Mo, wapeleke maombi yao ili yajadiliwe.

Sehemu ya wazee wa Simba waliohudhuria kikao hicho

Kwa majuma kadhaa sasa kumekuwa na mijadala mingi baina ya wanachama wa Simba wengi wakitaka Mo apewe timu lakini imeonekana kuwa jambo hilo ni gumu na linalohitaji mchakato ndipo uongozi wa klabu ulipoamua kuwaita wazee ili kujadili suala hilo kwani viongozi wa Simba walitamka kuwa hawakuwahi kupokea rasmi maombi ya MO zaidi ya kuyasikia kwenye vyombo vya habari.

''Kwa mfanyabiasha yoyote atakayetaka kuinunua Simba awe tayari kununua hisa chini ya 50% na si 51% kama anavyotaka MO, kwanza Simba ni taasisi ambayo ni kubwa ukilinganisha na kiasi anachotaka kutoa MO. Hiki kilikuwa ni kikao cha majadiliano lakini mwisho wa siku imeamuliwa kuwa itangazwe tenda na si kupeana tu.

''Hatujajadili suala la MO pekee bali na mambo mengine yenye kuleta maendeleo ndani ya Simba ikiwemo kuongeza mshikamano,'' alisema

Post a Comment

 
Top