BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanatarajia kwenda Afrika Kusini siku ya Ijumaa wiki hii ikiwa ni mwaliko wa maadhimisho ya miaka 25 ya moja ya klabu kongwe nchini humo. 


Yanga itatumia nafasi hiyo kujiandaa pia na michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo itaanzia ugenini nchini Maurituis ambapo mechi yao ya kwanza itachezwa Februari 14.

Kaimu Katibu mkuu wa Yanga,  Deusdedit Baraka yupo katika mchakato wa kuandika barua katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kuomba kusogezwa mbele kwa mechi zao za wiki hii.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro  amethibitisha kupokea mwaliko na kwamba kikosi chao kitashiriki michuano hiyo maalumu ikiwa ni moja ya maandalizi ya mashindano ya kimataifa.

"Tunaweza kuondoka muda wowote kwenda Afrika Kusini, hii ni kutokana na mwaliko tulioupata kutoka kwa klabu kongwe nchini humo.  katika hatua hizi za awali nisingependa kuitaja kwa jina kwanza, tutapata nafasi ya kucheza mechi za kirafiki kabla ya kwenda Mauritius," alisema Muro

Post a Comment

 
Top