BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
YANGA imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Yanga waliwashtukiza Friends kwa bao la mapema la dakika ya sita tu lililowekwa nyavuni na Simon Msuva akimalizia kwa kichwa mpira wa kona.

Baada ya bao hilo Yanga waliendelea kuliandama lango la Friends ambapo katika dakika 24, Msuva tena aliipatia bao la pili katika kwa shuti kali la nje ya 18.Dakika 29 kocha wa Friends Ally Yusuf 'Tigana' alimpumzisha Isihaka Hussein na nafasi yake ikachukuliwa na kinda Cliff Anthony ambaye alifanikiwa kuipa uhai Friends japo walishindwa kuzitumia nafasi chache walizopata kufunga mabao.

Kipindi cha pili Yanga iliingia kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika 51 likiwekwa kimiani na Matheo Anthony kwa kichwa.Kocha wa Yanga Hans Van Pluijm aliwapumzisha Msuva, Haruna Niyonzima na Issoufou Boubacar huku nafasi zao zikichukuliwa na Deus Kaseke, Yusuf Mhilu na Godfrey Mwashiuya. Kwa upande wa Friends, Tigana alifanya mabadiliko mengine kipindi cha pili kwa kuwatoa Good Hamis na Eliuter Mpepo akiwaingiza Mgaya Juma na mkongwe Mohamed Banka.

Kwa ushindi huo Yanga inaungana na watani zao Simba ambao jana waliifunga Burkina Faso mabao 3-0, kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Post a Comment

 
Top