BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, Dar
TIMU ya soka African Lyon imefanikiwa kurudi Ligi Kuu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya  Ashanti United. 


Mechi hiyo ilianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana lakini African Lyon ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao kupitia kwa mshambuliaji wao Omary  Abdallah. 

Kipindi cha pili Ashanti walirudi na kasi mpya huku wakipeleka mashambulizi ya nguvu langoni mwa Lyon ambapo dakika ya 50, Mwina Ally alifanikiwa kuisawazishia timu yake ya Ashanti na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare huku Lyon ikifikisha pointi 47.

Kocha wa Africa Lyon Salvatory Edward alisema "Mechi ilikuwa ngumu tunashukuru tumepata matokeo haya ya sare ambayo yametuvusha nawapongeza wachezaji wangu pamoja na viongozi kwa ushirikiano waliouonyesha,"

Post a Comment

 
Top