BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally. Shinyanga
MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib amesema kuwa endapo watani zao Yanga watathubutu kumpanga Vincent Bossou waandike maumivu kwenye mechi yao ya ligi lakini akipangwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ basi atakuwa na kazi ya ziada ya kutafuta mbinu za kumtoka.Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa wikiendi ijayo ya Februari 20 katik Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu zote zipo kwenye nafasi ya kuwania ubingwa.

Yanga nao wameshituka juu ya mbinu za Simba na tayari Cannavaro anatarajia kuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kuanza mazoezi mepesi kwani kwa mechi ambazo alikosa pengo lake lilionekana.

Ajib aliiambia BOIPLUS kuwa kutokana na uzoefu wa Canavaro kwenye safu ya ulinzi ya Yanga mchezo utakuwa mgumu ukilinganisha na Bossou ambaye ni mgeni.

“Natamani yule beki wao raia wa Togo anayevaa jezi namba 9 (Bossou) apangwe na kwenye mchezo wetu. Yule ni mlinzi mwepesi kumpenya na kusababisha madhara langoni mwa Yanga, tofauti na Cannavaro ambaye ni kisiki kumtambuka.

“Licha ya hivyo, Cannavaro ni mtu mwenye uzoefu wa hali ya juu kutokana na kufahamu vyema presha za michezo kama hii, hivyo uwepo wake kutafanya mchezo kuwa mgumu kutokana na kufahamiana vyema," alisema Ajib

Ajib alisema kocha wao Jackson Mayanja, amekuwa mwenye mipango mizuri na anakuwa na mbinu mpya kwa kile mechi hivyo Yanga wasitarajie kuoata ushindi kirahisi.

Timu hizo kwasasa zimepania kila mmoja kumfunga mwenzake kwani mzunguko wa kwanza Simba ililala kwa mabao 2-0.

Post a Comment

 
Top