BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MABINGWA wa Kombe la Kagame, Azam FC leo wametwaa ubingwa wa michuano ya kirafiki ya kimataifa  iliyoandaliwa na mabingwa wa Ligi Kuu Zambia, Zesco baada ya kutoka sare tasa na Zanaco.


Azam wametwaa ubingwa baada ya kuwa na mabao mengi ya kufunga kuliko wapinzani wao Zanaco, michuano hiyo ilikuwa ikifanyika katika Uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola.

Azam walikwenda kushiriki michuano hiyo kwa mwaliko maalumu ambapo timu nne zilishiriki kwao ikiwa ni moja ya maandalizi yao ya michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho.

Azam watalazimika kurudi nchini kuendelea na mechi zao za Ligi Kuu Bara ambapo ina kiporo cha mechi mbili huku ikiwa na pointi 39 sawa na Simba ambao wanashika nafasi ya tatu wakati Yanga ipo kileleni kwa pointi 40.

Post a Comment

 
Top