BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila AllyAZAM FC leo imetinga hatua ya robo fainali Kombe la FA na kuwafuata vigogo wa soka nchini Simba na Yanga baada ya kuifunga Panone FC bao 2-1. Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Ushirika jijini Moshi.

Mabao ya Azam yalifungwa na Pascal Wawa pamoja na Allan Wanga wakati Panone inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza imepata bao la kufutia machozi kupitia mchezaji wao Godfrey Masubugu.

Kwa matokeo hayo Azam itasubiri ratiba ya robo fainali ili kujuwa itacheza na nani huku tayari timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ni Coastal Union, Ndanda, Mwadui na Prisons.

Azam watatakiwa kurejea haraka jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga ambayo tayari imekwenda Pemba kwa ajili ya mchezo huo.

Post a Comment

 
Top