BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally

WACHEZAJI wa Coastal Union jana Alhamisi walitishia kugomea kucheza mechi ya leo ya Kombe la FA dhidi ya Mtibwa Sugar, kama wasingelipwa mishahara yao ya miezi miwili lakini jana hiyo walilipwa na leo wameiondoa Mtibwa kwenye michuano hiyo kwa ushindi wa bao 1-0.

Coastal waliingia uwanjani wakiwa na morali ya hali ya juu baada ya uongozi wao kuwalipa mishahara ya miezi miwili hapo jana. Mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Coastal ni timu ya pili kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ikitanguliwa na Yanga ambao waliifunga Mlale JKT bao 2-1.


Bao pekee la Coastal Union lilifungwa na Adeyun Saleh,  Coastal sasa watasubiri hatua ya robo fainali baada ya mechi zote za 16 bora kumalizika.

Post a Comment

 
Top