BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba
MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Rashid Mandawa yupo nchini Vietnam akifanya majaribioya wiki mbili katika Klabu ya Dongtam An Long FC inayoshiriki Ligi Kuu Vietnam .


Mandawa maarufu kama Chidikidebe ameiambia BOIPLUS kuwa awali hali ya hewa ya nchini humo ilikuwa ikimsumbua lakini kwasasa ameweza kuzoea hali hiyo.

"Mambo yanaenda vizuri na ninakaribia kurudi nchini Tanzania tatizo lililonikabili mwanzo ni hali ya hewa ila sasa nimezoea," alisema Mandawa

Endapo Mandawa atafanikiwa kwenye majaribio hayo atakuwa mchezaji wa tatu akiwemo Nizar Khalfan na Danny Mrwanda ambao waliwahi kuichezea Al Tadoon ya nchini humo.

Post a Comment

 
Top