BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MSANII mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kassim Mapili amekutwa amefariki nyumbani kwake Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam.


Habari za kifo chake zimejulikana usiku huu baada ya majirani kutomuona siku mbili na kutia mashaka, ndipo walipoamua kuvunja  mlango wa nyumba yake na kukuta mwili wake.

Inasemekana kwa mara ya mwisho  Mzee Mapili ambaye alikuwa akiishi peke yake nyumbani kwake ni juzi  aliposhuhudia mechi ya  Arsenal na Barcelona akiwa na majirani zake.

Shuhuda mmojawapo amesema mwili hauko katika hali nzuri na juhudi za kuwatafuta ndugu zake zinaendelea huku ikielezwa kuwa Mzee Mapili alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo.

Post a Comment

 
Top