BOIPLUS SPORTS BLOG

BONDIA Mtanzania, Francis Cheka ameibuka na ushindi kwa kumpiga Geard Ajetovic kwa ushindi wa pointi huku majaji wote wakimpa ushindi. Sasa ndiye bingwa mpya wa mabara, ubingwa ambao aliupoteza kwa kupigwa nchini Russia mwaka 2014.Ajetovic raia wa Serbia anayeishi nchini Uingereza alipinga baada ya kudai ndiye alicheza vizuri zaidi.

Katika pambano hilo kuwania ubingwa wa Mabara, Cheka alionekana kupiga ngumi nyingi za kudokoa lakini hazikuwa na nguvu sana kama za mpinzani wake aliyepiga ngumi chache lakini kali.

Mashabiki wengi waliokuwa kwenye Viwanja vya Leaders walionekana kuwa na hofu kutokana na Ajetovic kuachia ngumi kali za kushitukiza ingawa Cheka alipiga nyingi zaidi za kudokoa zilizomsaidia kupata pointi nyingi.

Hata hivyo, inawezekana ngumi nyingi za kudokoa ndiyo zilizompa ubingwa huo Cheka dhidi ya Ajetovic ambaye alionekana hatari kwake tokea mwanzo.

Source: Saleh Jembe

Post a Comment

 
Top