BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba kwa msaada wa Mitandao
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Memphis Depay jana alipelekwa katika timu ya umri wa chini ya miaka  21 na  kuisaidia kuibuka na ushindi  wa mabao 7-0 dhidi ya Norwich.


Katika mchezo huo Depay alifanikiwa kutoa pasi tatu za mabao huku mashabiki wengi wa United wakimpogeza sana kwa kiwango alichokionesha huku muda  wote akionekana mwenye furaha.

Kinda wa England Will Kean ndo aliongoza mashambuluzi ya United  na kufanikiwa kufunga mabao matano jana .


Wachezaji  wa timu ya  wakubwa waliojumuika  na timu hiyo ya vijana jana walikuwa ni Romero, Januzaj , Phil Jones,  Pereira  na Depay mwenyewe.


Kocha mkuu wa United, Luis Van Gaal alikuwepo uwanjani kuwashuhudia vijana hao ambao ndio watakuja kuisaidia timu ya wakubwa hapo baadae.

Post a Comment

 
Top