BOIPLUS SPORTS BLOG

TIMU ya Taifa ya Jamhuri ya Kidekrasia ya Congo (DRC) imetinga Fainali ya michuano ya Ubingwa wa mataifa ya Afrika (CHAN)
baada ya kuifunga Guinea kwa penalti 5 -4 Kufuatia sare ya 1-1ndani ya 120 za mchezo katika uwanja wa amahoro  mjini kigali, rwanda DRC iliyowatoa wenyeji Rwanda  Rwanda katika
Robo Fainali kwa kuwachapa mabao 2-1 baada ya dakika 120 pia ya kwanza kupata bao dakia 103 kupitia kwa mchezaji wao Jonathan Boling aliyemalizia pasi ya Guy Lusadisu.

Hata hivyo, Guinea iliyowatoa Zambia kwa mikwaju ya penati 5-4 Kufuatia sare ya 0-0katika dakika 120 pia, ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Ibrahima Sory

Katika mikwaju ya penalti, Badou
Bompunga, Mika Mhiche, Jonathan
Bolingi, Doxa Gikanji na Elia Meschack
wote walifunga upande wa DRC.  Huku waliokosa ni Ricky Tulengi na Jose Lomalisa Mutambala.

Upande wa Guinea waliofunga penalti ni Ibrahima Sankhon, Aboubacar Leo
Camara, Aboubacar Kile Bangoura na
Daouda Camara, wakati Ibrahima Sory
Bangoura, Mohamed Thiam na
Mohamed Youla walikoa.DRC, mabingwa wa CHAN ya kwanza
mwaka 2009 nchini Ivory Coast sasa
watasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya
pili kesho kati ya Mali na Ivory Coast katika Uwanja wa Nyamirambo kuanzia Saa
10:00, ili wakutane naye katika fainali.

Mali iliwastaajabisha wengi kwa
kuwatoa mabingwa wa mwaka 2011,
Tunisia kwa kuwachapa mabao 2-1,
wakati Ivory Coast iliwatoa Cameroon
kuwa kuwatandika mabao 3-0.

Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa
tatu wa michuano hiyo ya nne, baada
ya iIe ya 2009 Ivory Coast, 2011 Sudan
na 2014 Afrika Kusini ambako Libya
waliibuka mabingwa, zitafanyika
Jumapili.

Chanzo cha habari: BBC SPORTS

Post a Comment

 
Top