BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar

KAMATI ya Utendaji ya Klabu ya Simba imemsimamisha nahodha wake msaidizi Hassan Isihaka kuichezea klabu ya Simba kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya beki  huyo kumtolea maneno yasiyo na staha kocha wa Simba Jackson Mayanja kabla ya mechi ya jana Jumapili ya kombe la FA dhidi ya Singida United ambapo Simba ilishinda bao 5-1, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kutokana na kitendo hicho kisicho cha kiungwana kilichofanywa mbele ya wachezaji wenzake na kinachokiuka waraka wa maadili (code of conduct), Kamati ya utendaji licha ya kumsimamisha mchezaji huyo pia imeagiza alipwe nusu mshahara katika kipindi chote cha adhabu yake.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Simba, Haji Manara, imewataka wachezaji wote kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote wanapoitumikia klabu ya Simba.

Post a Comment

 
Top