BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi wetu, Shinyanga
SIMBA leo imefanikiwa kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom na kuishusha Yanga baada ya kuifunga Stand United mabao 2-1.


Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ilikuwa ni yenye ushindani mkubwa huku Simba iliyotumia nafasi zake vizuri imefanikiwa kufikisha pointi 45 wakati Yanga wao wana pointi 43 na mechi moja ya kiporo.

Mabao ya Simba yamefungwa na mganda Hamis Kiiza katika dakika za 34 na 47 huku bao la kufutia machozi la Stand United likifungwa na Jacob Massawe katika dakika ya 90

Kwa mabao hayo mawili Kiiza amefikisha jumla ya mabao 16 akimzidi Hamis Tambwe kwa mabao mawili hivyo kuendelea kukisogelea kiatu cha dhahabu ambacho yeye mwenyewe aliwahi kusema hana haja nacho bali anataka Simba iwe bingwa.

Katika michezo mingine African Sports imeifunga Mgambo bao 1-0, JKT Ruvu imetoka sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar, Ndanda imeifunga Majimaji bao 1-0 na Mbeya City ikafanya kufuru kwa kuibamiza Toto Africans mabao 5-0 

Post a Comment

 
Top