BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Dar
ILE mechi ya kukata na shoka iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kati ya vigogo Simba na Yanga imewadia. Ni katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam hapo kesho Februari 20 ambapo vita ya mafahari wawili italisimamisha jiji zima huku gumzo likisambaa nchi nzima na nje ya mipaka.


BOIPLUS imewatafuta nyota na watu maarufu kadhaa kutaka kujua utabiri wao kuelekea mechi hiyo ambayo ndio kubwa na yenye msisimko zaidi kuliko mechi zote za ligi kuu. Fuatilia hapa waliyoongea.

JAMHURI KIHWELO 'JULIO' - Kocha, Mwadui Fc
"Mechi ngumu sana hiyo, mwisho wa siku hakuna mbabe, Simba 2-2 Yanga. Mabao ya Yanga yatafungwa na Donald Ngoma na Simon Msuva huku yale ya Simba ni Ibrahim Ajib na Hamis Kiiza"

THOMAS ULIMWENGU - Straika, TP Mazembe
"Bro hiyo game haina mbabe na hamtoshuhudia hata bao moja, ni bila bila"JERRY MURO - Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano, Yanga
"Yanga itashinda mabao 3-1. Mabao ya Yanga yatafungwa na Ngoma, Tambwe na Msuva. Hilo la Simba litafungwa na Kazimoto"

JAMAL KISONGO - Meneja wa mchezaji Mbwana Samatta
"Kuna mabao mawili tu kesho, Simba 1-1 Yanga. Wafungaji ni Tambwe na Kiiza"

KHALID CHOKORAA - Mwanamuziki, Mapacha Watatu Band
"Sorry kama nitakukwaza kwa utabiri wangu kaka, ila kiukweli Yanga hachomoki kesho. Mwisho wa game Simba 2, Yanga 1"MBWANA SAMATTA - Straika, KRC Genk, Ubelgiji
"Aaah!, BOI mimi sio mzuri sana lwenye prediction bwana, ila kesho ni sare ya mabao 2-2"

WILLIAM LUCIAN 'Gallas' - Kiungo, Ndanda FC
"Mechi itakuwa ngumu sana ila Ajib na Kiiza wataamua matokeo ya ushindi wa Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga"

ATHUMAN MACHUPA - Straika wa zamani, Simba
"Matokeo yapo wazi hapo kaka, Simba 3-0 Yanga. Wafungaji ni Mkude, Ajibu na Kiiza"SHEKHAN RASHID - Kiungo wa zamani, Simba
"Hakuna mshindi hapo kaka, Simba 2-2 Yanga, mabao yatafungwa na Ngoma, Msuva kwa upande wa Yanga wakati yale ya Simba yatafungwa na Ajibu na Kiiza"

JUMA NATURE 'QIBRA' - Msanii wa mziki wa kizazi kipya
"Simba wanakaa mabao 2-0, hiyo haina kuwaza sana. Msuva na Ngoma ndio washereheshaji" JUMA LUIZIO - Straika, ZESCO, Zambia
"Kaka me naona suluhu tu hapo, hakuna mabao kabisa"

SWEDDY MKWABI - Mfanyabiashara 
"Ajib na Ugando watatufurahisha Msimbazi, mwisho wa siku Simba 2-0 Yanga"

RICHARD AMATRE - Kocha
"Mechi hiyo ni ngumu sana kuitabiri, ila haitokuwa na mabao mengi kama wengi wanavyodhani. Kutakuwa na bao moja au mawili tu"


ABRAHAM CHOVE - Kipa, Ndanda FC
"Mechi za hao jamaa huwa ni ngumu bila kujali nani yuko vizuri. Kwa game ya kesho matokeo ni sare ya bila mabao"

RAZACK CARECA - Straika wa zamani, Coastal Union
"Mechi za Simba na Yanga ni ngumu lakini kwa kesho Simba atashinda bao 1-0, Ibrahim Ajib ndio mfungaji"

LUBIGISA MADATA - Beki wa zamani, Simba
"Hamis Kiiza atafunga mabao mawili huku Ajib akifunga moja na kuipatia Simba ushindi wa mabao 3-0"Post a Comment

 
Top