BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa Simba, Raphael Kiongera amerudi kwao kwa ajili ya kujisikilizia zaidi hali yake kwani anasumbuliwa na maumivu ya nyonga na kwa mujibu wa Daktari Gilbert Kadyage mchezaji huyo atalazimika kukaa nje kwa wiki tatu ili awe fiti kabisa.


Kiongera aliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita na amesema atarejea muda wowote kujiunga na nwenzake na tayari amemaliza wiki moja tangu alivyopelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Nitarudi huko muda wowote kuanzia sasa, maumivu yamepoa kidogo ila naamini nitakuwa vizuri muda si mrefu, hakuna dawa ninayotumia na wala sikufanya vipimo vyovyote zaidi Dr. Gilbert aliniangalia na kugundua tatizo, ninachofanya sasa hivi ni kupumzika na kufanya 'massage' hiyo ndio dawa pekee," alisema Kiongera.

 Kwa upande wa Dr Gilbert alisema kuwa, Kiongera anapaswa kufuata masharti ya kupumzika na kufanya 'massage' kwa umakini mkubwa vinginevyo tatizo lake litakuwa linajirudia na baadaye litamletea shida zaidi.

"Dawa ya tatizo lake ni kupumzika na kufanya 'massage' kwa nguvu bila kuzembea, akifanya uzembe kwenye hilo basi litampa shida, anatakiwa kupumzika kwa wiki mbili na wiki ya tatu ndipo aanze mazoezi mepesi, hakuna dawa ya kutumia labda lingekuwa tatizo kubwa sana," alisema Dr Gilbert

Post a Comment

 
Top