BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KIPA wa Prisons, Beno Kakolanya amesema kuwa yupo tayari kuondoka kwenye kikosi hicho na kutangaza ofa yake ya Sh 35 milioni kwa timu itakayomuhitaji.Beno anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu ambapo ameichezea timu hiyo kwa miaka mitatu sasa.

Akizungumza na BOIPLUS, Beno alisema kuwa umefika muda wa yeye kupata changamoto mpya kutoka kwenye timu nyingine ingawa ameweka wazi hata Prisons wakimpa dau hilo yupo tayari kubaki."Nimeishi na Prisons maisha mazuri ni timu nzuri na inafanya vizuri kwenye ligi ila soka ndiyo ajira yangu ndiyo maana nahitaji kupata changamoto mpya. Fedha ninayohitaji ni hiyo ila kuna mazungumzo kwani soka ni biashara inayohitaji kuelewana,"  alisema Beno

Beno ambaye ni kipa namba moja wa Prisons amecheza mechi nane kabla ya mechi ya leo Jumatano dhidi ya Azam Fc, mzunguko wa kwanza kipa huyo hakucheza mechi nyingi kwani alikuwa akisumbuliwa na bega.

Post a Comment

 
Top