BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
UONGOZI wa Gor Mahia leo umevunja mkataba na kocha mkuu wa timu hiyo, Frank Nuttall akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa miezi 16 tu.



Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Nuttall amesema chanzo cha kuvunjwa kwa mkataba huo ni kitendo cha uongozi wa Gor Mahia kutaka kumpunguzia mshahara wake kwa asilimia 50.

"Walitaka kunipunguzia mshahara kwa 50% wakati mkataba wangu unaeleza wazi kuwa kutakuwa na nyongeza ya asilimia 10 mwezi Januari mwaka huu." alisema Nuttall katika taarifa hiyo.

Mkataba wa Nuttall na Gor Mahia uliokuwa umalizike mwezi Januari 2017 umevunjwa huku kocha huyo akiwa ametoka kupata mafanikio makubwa na klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo KPL.



Nuttall amewashukuru wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano waliomuonyesha tangu ajiungenao mwezi Septemba 2014. 

Post a Comment

 
Top