BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
SIKU zote imekuwa ni kawaida kwa Simba na Yanga kwenda kupiga kambi yake visiwani Zanzibar hasa wanapoelekea kwenye mechi yao ya watani lakini kwa sasa ni tofauti, Simba itapiga kambi yake mkoani Morogoro wakati Yanga tayari wametua visiwani Pemba.


Simba imeondoka saa 5 asubuhi wakitokea Shinyanga ambako walikuwa na mechi zao mbili za Ligi Kuu Bara ambazo wameshinda zote na kuondoka na pointi sita, waliifunga Kagera Sugar bao 1-0 pamoja na Stand United bao 2-1.

Yanga wenyewe tayari wametua Pemba wakitokea Mauritius ambako walikuwa na mechi ya kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya ... ambayo wameifunga bao 1-0.

Kocha wa Simba, Jackson Mayanja aliiambia BOIPLUS kuwa "Siwezi kuzungumza chochote kuhusu mechi ya Yanga, nataka kujua kwanza wachezaji wangu wangapi wameumia kwasababu kuna wachezaji tuliwatoa kutokana na kuumia akiwemo Hassan Kessy, mambo yote kuhusu Yanga nitayazungumzia Jumatatu,"

Simba kwa sasa ipo kileleni ikiwa na pointi 45 wakati Yanga wao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 43 huku wakiwa na mechi moja ya kiporo mkononi ambapo mechi yao itachezwa Februari 20 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top