BOIPLUS SPORTS BLOG

KLABU ya Manchester City ya Uingereza imethibitisha kukamilisha mazungumzo na kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola ili ajiungenao mwishoni mwa msimu huu.


Guardiola na City wamekubaliana kusaini mkataba wa miaka mitatu utakaoanza mara baada ya kocha Manuel Pellegrin kumaliza kazi yake mwishoni mwa msimu huu.

Katika taarifa yao City wamesema kuwa Pellegrin ameshirikishwa kwa kiwango kikubwa katika mchakato huo na kwamba kwa sasa ameweka nguvu zake katika kuhakikisha anamaliza msimu huu kwa mafanikio. 

Post a Comment

 
Top