BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Shinyanga
KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amewatabiria washambuliaji wake Hamisi Kiiza raia wa Uganda na Ibrahim Ajibu kuwa mmoja atakuwa Mfungaji Bora wa msimu.


Tayari Kiiza amefikisha mabao 14 sawa na Amisi Tambwe wa Yanga huku Ajib yeye akiwa na mabao nane sawa na Kipre Tchetche wa Azam FC.

Mayanja alisema anawaamini wachezaji wake hao kuwa wanauwezo wa kufunga mabao mengi huku akiwataka kila mechi kufunga mabao mawili mawili kila mmoja.

"Wanatakiwa wakiingia uwanjani akili zao ziwe na lengo moja tu la kufunga, kila mechi wajipangie kufunga bao mbili na wasaidiane kuzitafuta kama Kiiza alivyofanya mechi iliyopita alimpa pasi Ajib na akafunga, ila naamini mfungaji bora atatoka kwangu kati ya Kiiza na Ajib," alisema Mayanja

Kuhusu mechi yao ijayo dhidi ya Stand United, Mayanja alisema "Mechi hiyo ni ngumu kuliko hata ya Yanga kwani anakutana na timu ambayo wachezaji wengi hawafahamu,".

Post a Comment

 
Top