BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MABINGWA wa soka barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo leo imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 pale ilipopambana na FC Tshinkunku katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa kwenye dimba la TP Mazembe jijini Lubumbashi.Mtanzania Thomas Ulimwengu alifanya kazi nzuri iliyomaliziwa nyavuni na Roger Assale katika dakika ya 16 ya mchezo na kuwafanya maelfu ya mashabiki wa Mazembe waliohudhuria mechi hiyo waanze kucheza 'Ekotite' mapema.

Kama alikuwa analipa fadhila, Assale alimpikia bao Ulimwengu katika dakika 23 huku hili likiwa ni bao lake la pili kwa mwaka huu katika michezo mitatu aliyoichezea timu hiyo tangu ajiungenayo akitokea mapumzikoni. Timu hizo zilienda mapumziko huku Mazembe ikiongoza kwa mabao hayo mawili.

Mazembe iliyoonekana kuizidi kila idara Tshinkunku, iliendeleza sherehe katika kipindi cha pili kwa mabao ya haraka haraka yaliyofungwa na Luyindama katika dakika ya 75 na  Rainford Kalaba dakika ya 76 na 84.

Hata hivyo, Ulimwengu alitolewa nje katika dakika ya 63 nafasi yake ikichukuliwa na Kalaba baada ya kupata maumivu. 

Baada ya mchezo huo Ulimwengu aliiambia BOIPLUS kuwa hakupata maumivu makali sana bali alitolewa tu kwa tahadhari ya kuumia zaidi.

Post a Comment

 
Top