BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Marco Ngavenga, Mbeya
TIMU ya Mbeya Warriors ya jijini Mbeya, imeinyuka timu ya Mkamba Rangers ya mjiji Morogoro mabao 3-1, katika mechi ya Ligi Daraja la pili iliyochezwa kwenye Uwanja Wa Sokoine jijini hapa.


Kwa ushindi huo, Mbeya Worriors imejihakikishia kupanda daraja baada ya kufikia pointi 19 huku ikiwa imebakiza mechi tatu ambapo inahitaji ushindi katika mechi moja tu kati ya hizo.

Katika kundi hilo, timu inayomfukuzia Mbeya warriors ina point 12 ambapo hata ifanye miujiza gani haiwezi kuifikia warriors.


Kwenye mechi yao dhidi ya Mkamba Rangers, Worriors ilijipatia mabao kupitia kwa wachezaji wake,  Kelvin Mwelela aliyefunga bao la kwanza, Jimson Steven aliyefunga bao la pili, huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Moi Mwasoni. 

Bao la kufutia machozi la Mkamba  lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa penati na nahodha wake, Stanslaus Mkachange.Post a Comment

 
Top