BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
MECHI mbili za viporo za Azam FC sasa zimepangiwa tarehe ambapo Mabingwa hao wa Kombe la Kagame wametamba kupambana ili kushinda mechi zao zote.


Kiporo cha kwanza cha Azam dhidi ya Prisons kitachezwa Februari 24 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati na Stand United itachezwaa Machi 16, Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mechi za Azam zilisogezwa mbele baada ya timu hiyo kwenda kushiriki michuano ya kirafiki ya kimataifa iliyoandaliwa na mabingwa  wa Ligi nchini humo, Zesco ambapo Azam walitwaa ubingwa huo.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Denis Kitambi amesema kuwa katika mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wamejipanga kuondoka na pointi tatu huku akiwataja Agrey Morris na Didier Kavumbagu kuwa wataikosa mechi hiyo kwani ni majeruhi.

"Tumejipanga na tutapambana na Coastal Unioni ili kupata pointi tatu lengo letu ni kushinda mechi zote zilizobaki," alisema Kitambi ambaye timu yake itaondoka keshokutwa Alhamisi kwenda Tanga.

Post a Comment

 
Top