BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
MCHEZAJI bora wa Dunia Lionel Messi amezima ndoto za Arsenal kuingia hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuifungia timu yake mabao mawili na kuifanya iibuke na ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Emirates jijini London.


Licha ya Barca kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa, bado walishindwa kupata bao hadi dakika ya 71 pale Messi alipoituma vema pasi ya kiufundi ya Neymar Dos Santos kutoka upande wa kushoto na kuiandika timu yake bao la kuongoza.

Baada ya bao hilo Arsenal walianza kupoteana hivyo kuwapa nafasi Barca ya kupachika bao jingine kupitia kwa Messi safari hii ikiwa ni kwa njia ya penati katika dakika ya 84.

Mchezo huo uliojawa na ufundi mwingi ulishuhudia kadi mbili tu za njano moja ikienda kwa Nacho Monreal  wa Arsenal na kuna  ya Gerald Pique huku Barca wakipata kona 7 huku Arsenal wakiambulia kona moja tu.

Huko nchini Italia, Juventus iliwakaribisha Bayern Munich ya Ujerumani na timu hizo kutoka kwa sare ya mabao 2-2. Mabao ya Bayern yalifungwa na Thomas Muller na Arjen Robben huku yale ya Juventus yakifungwa na Paulo Dybala na Stefano Sturaroi

Post a Comment

 
Top