BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba kwa msaada wa mitandao
WIKI iliyopita mashabiki wa Liverpool waliamua kutoka uwanjani  dakika ya 77 katika mchezo dhidi ya Sunderland wakipinga bei mpya za tiketi iliyopangwa kutumika msimu 2016/17.


Baada ya tukio hilo wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group ambao ni John W. Henry, Tom Warner na Mike Gordon wameamua kuandika barua ya kuwaomba radhi mashabiki hao kutokana na mpango wao wa kupandisha bei ya tiketi.

Sehemu ya barua hiyo ilisomeka hivi.
"Sisi kama wamiliki tunadiriki kuomba radhi kwa mashabiki kwa mpango wetu  wa kupandisha bei ya tiketi za msimu wa 2016/17 , hakika hii ilikuwa wiki mbaya sana kwetu Fenway Sports Group na hii ilionesha sisi hatujali mashabiki na ni wachoyo na  tunaojijali wenyewe ."


Baada ya tukio hilo, wamiliki hao wa Liverpool wameamua kukutana na viongozi wa mashabiki wa Liverpool na kuafikiana kushusha na kuendelea kuwajali mashabiki wao.  Waziri Mkuu wa Uingereza, David  Cameroon pia alitia neno katika hili kwa kusema inabidi kifanyike kitu ili kupunguza kupanda kwa kasi kwa bei ya tiketi.

Post a Comment

 
Top