BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba
WIKI iliyopita beki wa Coastal Union, Ernest Mwalupani alifunga ndoa na Upendo Mbyopyo ambaye alimshawishi kunyoa rasta zake alizokaa nazo kwa miaka mingi na hivyo aliingia kanisani akiwa na mwonekano mpya tofauti na alivyokuwa amezoeleka uwanjani.


Mwalupani aliiambia BOIPLUS kuwa alinyoa rasta zake wakati wa maandalizi ya harusi yake hiyo kutokana na maandalizi ya harusi yake ingawa kwake ilikuwa ni vigumu kukubaliana na maamuzi hayo ya kufyeka rasta hizo.

"Ilinibidi nikubali kunyoa rasta ili niendane na shughuli ya heshima iliyokuwa mbele yangu kwani wengi wanachukulia rasta kama uhuni fulani hivi. Rafiki zangu wengi walinikataza kunyoa kwa madai kuwa nitapoteza utambulisho wangu lakini mke wangu alipoaniambia ninyoe nilisikiliza na kuzinyoa," alisema Mwalupani


Mwalupani alisema kuwa siku hiyo ilikuwa muhimu kwake na mke wake ambao walidumu katika uchumba kwa miaka 11 mpaka walipoamua kufunga ndoa na kuingia katika ulimwengu mpya wa kutengeneza familia.

Post a Comment

 
Top