BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MARA nyingi timu za jijini Dar es Salaam hasa Simba, Yanga na Azam zimekuwa zikilalamikia ubovu wa viwanja vya mikoani. Hii ni kweli ingawa kuna vyenye afadhali na kuna vile ambavyo havitazamiki. 


Huu ni Uwanja wa Majimaji uliopo Songea mkoani Ruvuma unaotumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara mpaka sasa. Azam Fc walishacheza hapa na kupata pointi tatu 'kigumugumu'.


Sasa unaonekana kujaa maji, mashimo na sehemu nyingi hauna nyasi, upo kama majaruba ya mpunga. Simba na Yanga ni moja kati ya timu zinazotarajiwa kucheza katika uwanja huu katika mzunguko wa pili unaoendelea.


Post a Comment

 
Top