BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
KIUNGO wa Simba, Mwinyi Kazimoto kesho Juamatatu anatarajia kupandishwa kizimbani kujibu shitaka lake la kumshambulia mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Mwanahiba Richard.Mwinyi alimshambulia Mwandishi huyo Februari 10, mwaka huu wakati Simba ikiwa mkoani Shinyanga ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ambapo alifanya shambulizi la kudhuru mwili kwa kumpiga makofi na ngumi tukio lililofanyika baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kambarage.

Mwinyi anatarajiwa kufikishwa kujibu shitaka hilo katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga saa 2:00 asubuhi, hiyo ni baada ya faili kurudishwa kutoka kwa Mwanasheria wa Serikali katika kituo cha Polisi ilipofunguliwa kesi hiyo na kubaini kwamba kuna kosa linalostahili kupelekwa mahakamani.

Jana Jumamosi, kiungo huyo aliichezea timu yake ilipopambana na Yanga na kufungwa mabao 2-0 huku yeye akipumzishwa kipindi cha pili.

Post a Comment

 
Top