BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo Jumatano wameendeleza ubabe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Mlale JKT bao 2-1, mechi ambayo imechezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.JKT Mlale ndiyo walikuwa wa kwanza kuona lango la Yanga katika dakika ya 21 kupitia mchezaji wao Mgandila Shabani baada ya kuwatoka mabeki na kupiga shuti lililotinga nyavuni.

Dakika ya 33, Simon Msuva aliikosesha Yanga bao baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba na kurudi ndani ya uwanja akipokea pasi ya Mwashiuya ambapo wachezaji wa Mlale waliokoa.

Hata hivyo, Yanga walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 38 ambalo lilifungwa na Paul Nonga akipokea krosi ya Mwashiuya.

Dakika ya 39, kiraka Mbuyu Twite alikosa bao baada kuoiga shuti refu nje ya 18 ambalo lilitoka nje kidogo ya goli.

Kipindi cha kwanza Yanga ilipata nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia vyema ikionekana wazi kulikuwa na matatizo ya umaliziaji hasa kwa washambuliaji wake Matheo Anthony, Nonga na Mwashiuya.Kipindi cha pili, kocha wa Yanga, Hans Pluijm aliamua kumtoa nje Matheo nafasi yake ilichukuliwa na Donald Ngoma lengo ni kuongeza idadi ya magoli kutokana na umahiri wa straika huyo raia wa Zimbabwe katika kuzifumania nyavu.

Dakika ya 54, Salum Telela alilazimika kutolewa nje baada ya kugongana na mchezaji wa Mlale JKT wakati anawania mpira wa juu ambapo watu wa huduma ya kwanza walimtoa kabisa uwanjani na kumpeleka chumba maalumu kwa ajili ya matibabu.

Thaban Kamusoko alichukuwa nafasi ya Telela ambapo aliipatia Yanga bao la pili dakika ya 58 akipokea krosi ya Mwashiuya huku Pluijm akimtoa Nonga na kumuingiza Malimi Busungu ikiwa ni dakika ya 59.

Mwamuzi Israel Mujuni alitoa kadi nyingine ya njano kwa mchezaji wa JKT Mlale, Othuman Muhagama aliyemchezea rafu Twite.

Kwa matokeo hayo, Yanga imefuzu hatua ya robo fainali ingawa bado haijajulikana itacheza na nani mpaka hapo ratiba itakapopangwa.

Post a Comment

 
Top