BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Marco Ngavenga, Mbeya
TIMU za Tanzania Prisons na Azam Fc leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye dimba la Sokoine hapa jijini MbeyaKipindi cha kwanza kilianza kwa mashambulizi kadhaa huku Azam wao wakitawala mpira kwa asilimia kubwa zaidi na kulishambulia lango la Prisons mara kwa mara. Hata hivyo washambuliaji wake John Bocco, Ramadhani Singano na Kipre Tchetche hawakuwa makini kukwamisha mipira nyavuni.

Mechi hiyo ambayo haikuwa na msisimko mkubwa ukilinganisha na ile iliyochezwa jumamosi iliyopita kati ya Azam na Mbeya City, iliendelea katika kipindi cha pili kwa kosakosa za mabao na kuwafanya mashabiki waliohudhuria wakose burudani waliyoitarajia.
Hadi  mwisho wa mchezo timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare isiyo na mabao.Kwa matokeo hayo Azam imejizolea pointi nne jijini Mbeya na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwa pointi 46 sawa na Yanga inayoongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Simba inashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 45.

Post a Comment

 
Top