BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kupoteza mechi dhidi ya Coastal Union kumewaharibia mipango yao lakini wametamba kuwa katika nafasi nzuri ya kurekebisha makosa dhidi ya mechi yao ya kesho Jumatano na Prisons ambao pia wametamba kubaki na pointi tatu.


Mbali na mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Yanga ambayo bado inashikilia usukani wa ligi ikiwa na pointi 39 wameapa kufanya vizuri kwenye mechi zoa zote zilizobaki.

Mwambusi alisema kuwa mpira una mambo mengi ikiwemo matokeo matatu kushinda, kufungwa na kutoka  sare huku akiweka msisitizo wa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

"Kwa mtu mwenye malengo si jambo zuri kupoteza mechi lakini tunaamini tutakirekebisha mechi zilizobaki na kutetea ubingwa," alisema Mwambusi.


Wakati Yanga wakutamba kuifunga Prisons, kocha mkuu wa Wajelajela hao Salum Mayanga amesema kuwa anawasubiri Yanga kwani naye lengo ni kuifikisha timu yake katika nafasi bora za juu.

"Sina shaka na kikosi changu, tumejipanga na nimejiwekea malengo ya kuwa Prisons inakuwa miongoni mwa timu tano bora za juu. Kwetu hakuna mechi rahisi zote ni ngumu, Yanga si timu mbaya na tunaiheshimu ila kesho tumepanga kubaki na pointi tatu, nafahamu watakamia kwani wamepoteza mechi yao iliyopita," alisema Mayanga.

Post a Comment

 
Top