BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
STRAIKA na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta leo ameifungia bao lake la kwanza timu hiyo aliyojiunganayo mwezi Januari akitokea TP Mazembe ya DR Congo. Samatta ambaye huanzia benchi katika michezo yote, leo aliingia katika dakika ya 79 ya mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji dhidi ya vinara Club Brugge akichukua nafasi ya Nikos Karelis ambaye aliipatia Genk bao la kwanza dakika ya 36 kwa mkwaju wa penati kabla Thomas Buffel hajatupia la pili kwenye dakika ya 50.

Dakika mbili tu tangu aingie uwanjani, Samatta alifungua rasmi kitabu chake cha mabao kwa goli safi alilofunga kwa utulivu mkubwa akiwa mbele ya kipa wa Brugge katika dakika ya 81.

video
Tazama video ya bao la Samatta

Mabao ya Brugge inayoendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 58 sawa na Gent inayoizidi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, yaliwekwa nyavuni na Thomas Meunier katika dakika ya 15 na Hans Vanaken dakika 83.

Kwa ushindi huo Genk wanaendelea kubaki katika nafasi ya tano kwa kujikusanyia pointi 45 ikiwa ni pointi moja tu nyuma ya Oostende inayoshika nafasi ya nne.

Post a Comment

 
Top