BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda

MBWANA Samatta leo amefunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na klabu ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji. Ni bao muhimu ambalo limeisaidia timu yake kuondoka na pointi tatu dhidi ya vinara wa ligi hiyo Club Brugge.

Katika mahojiano na BOIPLUS ambayo ilimtafuta mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ili kujua anajisikiaje baada kufungua kitabu cha mabao barani Ulaya, Samatta alisema amefurahi sana kwavile hicho ni kitu ambacho amekuwa akikiwaza tangu alipotua nchini Ubelgiji. 

"Najisikia furaha sana, ni kitu nilichokuwa nakifikiria toka nimefika lakini baada ya kukipata kinageuka kuwa changamoto kwangu kwani nahitajika kufanya hivyo kila wikiendi. Kwahyo inabidi nijitume zaidi ili niweze kufunga kila wakati." alisema Samatta

Mtoto Karim Mbwana Samatta (1)

Samatta aliongeza kwa kusema analitoa bao lake hilo muhimu na la kihistoria kwake kama zawadi kwa mtoto wake wa mwaka mmoja aitwaye Karim.

"Bao hili lenye umuhimu wa kipekee kwenye historia ya soka langu ni dedication kwa mwanangu Karim kama yeye alivyo na umuhimu wa kipekee kwangu."

Post a Comment

 
Top