BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Shinyanga
SIMBA imezoa pointi tatu za ugenini baada ya kuifunga Kagera Sugar bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoni Shinyanga.Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 42 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara huku Yanga wakifikisha pointi 43 na kubaki kileleni.

Bao la Simba lilifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 44 akipokea krosi ya Hamis Kiiza ambaye baadaye kocha wa Simba Jackson Mayanja aliamua kumtoa baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi nafasi yake ilichukuliwa na Brian Majwega.

Simba ilifika mara nyingi langoni mwa wapinzani wao lakini kukosa umakini kuliwakosesha mabao mengi huku Mayanja akiwatoa pia Hija Ugando na Mwinyi Kazimoto nafasi zao zilichukuliwa na Danny Lyanga na Emery Nimubona.

Kocha wa Kagera Sugar, Adolf Rishard naye alifanya mabadiliko ambapo aliwatoa Martin Lupart, Mbaraka Yusuph na George Kavila aliyeumia nafasi zao zilichukuliwa na Babu Ally, Idd Kurachi na Ramadhan Kiparamoto.

Simba ilipata penalti dakika ya 83 baada ya Ajibu kuangushwa eneo la hatari ambapo Ajibu alilazimika kupiga penalti hiyo lakini kipa wa Kagera Sugar, Andrew Ntala alipangua.

Mwamuzi wa mchezo huo, Mathew Akrama kutoka Mwanza alitoa kadi nyekundu dakika ya 90 kwa mchezaji wa Kagera Sugar, Jumanne Daudi kwa kile kilichoelezwa ni kumjibu vibaya mwamuzi huyo.

Kadi nyingine za njano zilikwenda kwa Job Ibrahim baada ya kumchezea rafu Mwinyi Kazimoto pamoja na Abdi Banda naye alipewa kadi hiyo.

Simba wataendelea kuwepo mkoani Shinyanga wakisubiri mechi yao dhidi ya Stand United itakayochezwa Jumamosi ya wiki ijayo kabla hawajarudi Dar es Salaam kucheza na Yanga.

Matokeo ya mechi zingine:
JKT Ruvu 0-4 Yanga
Azam 1-0 Mwadui
Mbeya City 0-0 Prisons
Ndanda 1-1 Mtibwa
Majimaji 1-0 Mgambo

Toto Africans 2-1 Coastal

Post a Comment

 
Top