BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KLABU ya Simba leo imezindua duka la vifaa mbalimbali ambavyo si jezi ambalo lipo katika jengo la Dar Free Market, jijini Dar es Salaam.


Uzinduzi huo umefanywa na Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye aliwashukuru EAG ambao ni kampuni iliyoingia mkataba kwa ajili ya masuala ya masoko ya klabu hiyo ambao walibuni mradi huo.

Aveva alisema kuwa wataendelea kufungua maduka zaidi katika ya jiji na baadaye kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania ili mtu yeyote aweze kujipatia vifaa hivyo ambapo mapato yatakuwa yanaisadia klabu kwenye matumizi mbalimbali.


"Nawashukuru EAG ambao tuliingia nao mkataba mwaka jana, walianza na kazi ya jezi na leo hii tunazindua duka linalouza vifaa mbalimbali ambavyo si jezi, duka lilingine tutafungua Makao Makuu ya klabu na baaye sehemu zingine za jiji na nje ya mji," alisema Aveva.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa EAG, Imani Kajula alisema kuwa "Hivi vifaa pia vitakuwa vinatapatika kwa njia ya mtandao kama ilivyokuwa wakati wa uuzaji wa jezi zetu, kwani wadau wengi pia walinunua jezi kupitia mtandao,".

Post a Comment

 
Top