BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe na Hamisi Kiiza wa Simba wapo kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiatu cha Dhahabu lakini Tambwe amemwambia Kiiza akae pembeni kwani hawezi kutwaa kiatu hicho japokuwa amemzidi goli moja.


Mpaka sasa Kiiza amefikisha mabao 16 huku Tambwe akiwa na mabao 15 na amejipa matumaini makubwa ya kutwaa kiatu hicho ambacho amewahi kukibeba wakati huo anaichezea Simba alipofika mabao 17.

Akizungumza na BOIPLUS, Tambwe alisema kuwa "Nitaendelea kupachika mabao kwasababu napata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzangu pamoja na viongozi wangu hivyo huyo Kiiza awe tayari kutoka kileleni

"Simba waliniacha kwa madai kuwa kiwango changu kimeshuka ila nawadhihirishia kuwa nipo vizuri na ninashukuru nathibitisha hilo hata kwenye mechi tunazokutana nao, wanajisifu wana safu nzuri ya ulinzi na hawajafungwa mechi sita ila sisi tumewafunga, nikiamua jambo hakuna anayeweza kunizuia, kama
nilivyoamua kuwafunga wao katika mechi hiyo ya juzi," alisema Tambwe

Post a Comment

 
Top