BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi 'Mido', JNIA
YANGA wamepaa mchana huu kwa ndege ya kukodi kuelekea nchini Mauritius kwenda kuikabili Cercle de Joachim katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika.

Kamera ya BOIPLUS ilikuwepo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) ili kukuletea kila kilichojiri.


 'Maafisa wa Idara ya Ulinzi'.....Kelvin Yondan na Juma Abdul wanaopaswa kuhakikisha hawafungwi bao lolote ugenini ili kurahisisha kazi katika mechi ya pili itakayopigwa jiji Dar


 'Mawinga Teleza'......Simon Msuva na Geoffrey Mwashiuya, wanatarajiwa kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni

Kipenzi cha wanajangwani, Haruna Niyonzima, amerejea kwenye mstari kuisaidia timu yake kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa


Straika Donald Ngoma....je, ataenda kuibeba Yanga yake ugenini?


 Mbuyu Twitte na Ally Mustafa 'Barthez' Paul Nonga nae yumo kwenye msafara ulioitwa wa kwenda 'kuwaua' wamauritius

Kocha mkuu Hans Van Pluijm akishuka kwenye basi kwenda kupanda ndege

Post a Comment

 
Top