BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
WAKATI Mbwana Samatta anatambulishwa rasmi kwa wachezaji wenzake wa KRC Genk na baadaye kufanya nao mazoezi kwa mara ya kwanza leo, pacha mwenzake wa Taifa Stars aliyemuacha katika klabu ya TP Mazembe, Thomas Ulimwengu 'Buffalo'  alikuwa anaichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu aliporejea akitokea kwenye mapumziko.


Watu wengi waliamini kuwa Ulimwengu angeweza kuathirika kisaikolojia baada ya Samatta kuondoka kutokana na ukaribu wa wawili hao walipokuwa nchini DR Congo, lakini hiyo imeonekana si tatizo baada ya Straika huyo kuifungia Mazembe bao dakika mbili tu tangu aingie uwanjani katika mchezo wa Ligi kuu nchini humo dhidi ya Tshinkunku.

Ulimwengu aliingia katika dakika ya 77 akichukua nafasi ya Luyindama na dakika ya 79 tu aliitendea haki pasi ya Given Singuluma na kuipatia Mazembe bao la nne na la mwisho katika mchezo huo ulioisha kwa Mazembe kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 jijini Lubumbashi.


Mabao mengine ya Mazembe yalifungwa na Luyindama (13), Singuluma (41) na Awako (73).
Katika mchezo ujao wa February 3, Mazembe itaikaribisha JS Groupe Bazano katika uwanja wao aa nyumbani.

Post a Comment

 
Top