BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
WACHEZAJI wa Coastal Union leo walivamia ofisi za klabu yao zilizopo jijini Tanga ili kushinikiza walipwe mishahara yao.


Wachezaji hao wanaudai uongozi wao mishahara ya miezi mitatu huku wakidai kuwa wanaweza kugoma kucheza mechi yao ya kesho Ijumaa dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo ni ya Kombe la FA itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Wachezaji hao wanashinikiza kulipwa mishahara hiyo huku wakidai kuwa maisha yamekuwa magumu kwao na wamekuwa wakijitolea bila viongozi kujali lolote.

"Ni kweli hatujalipwa mishahara miezi mitatu sasa, kila siku wanatuahidi tu ila hawatekelezi tumechoshwa na tabia hizo kwani tuna familia zinatutegemea, hatuna uhakika kama kesho tutaingia uwanjani wasipotulipa," alisema mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.

Habari zaidi zinasema kuwa viongozi hao walikuwa na mpango wa kukutana na wachezaji wao mchana wa leo ili kutatua tatizo hilo.

Mwenyekiti za Coastal Union, Dr Ahmed Twaha alisema kuwa atalizungumzia hilo jioni kwani mazingira aliyokuwepo hayakumruhusu kuzungumza na simu.

Post a Comment

 
Top