BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Swabri Kachwamba
BAADA ya kukaa nje uwanja kwa takribani miezi 10, Dany Welbeck leo amerudi na kufunga goli dakika ya 90 (5)  na kuisadia Arsenal kuibuka na pointi tatu muhimu.


Walikuwa ni Leicester walioanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Jamie Vardy aliyefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 45 na kuifanya Leicester kwenda mapumziko wakiongoza.

 Kipindi cha pili kocha Arsene Wenger aliwaingiza Chambers , Theo Walcott na Danny Welbeck kitu kilicho waongeza nguvu Arsenal na kuweza kusawazisha kupitia kwa Walcott katika dakika ya 70 na baadae Welbeck (90+5) na kuwafanya Arsenal kupunguza tofauti ya pointi kati yake na Leicester na sasa ikizidiwa kwa pointi mbili tu.


Katika mchezo huo kiungo mkabaji wa Arsenal Francis Coquilin nae alirudi kutoka katika majeruhi ya muda mrefu.

Kikosi cha Leicester kilichoanza ni
Scheimeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy .
Walioingia baadae ni King, Gray na Wasilewski.


Kikosi cha Arsenal kilichoanza leo ni Cech, Bellerin, Martesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Oxlade -Chamberlin, Ozil,  Alexis na Giroud  .

Walio ingia badae ni
Chambers  ,Walcot na Welbeck

Post a Comment

 
Top