BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi wetu, Curepipe
YANGA 'walidondoka' Mauritius jana usiku, leo wakaamka kujiandaa kwenda uwanjani na bila kujiuliza wakaipiga Cercle de Joachim bao 1-0. Baada ya hapo kinachofuata ni kupaa zao kwa ndege ya kampuni ya ATC kuelekea kambini visiwa Pemba.


Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni na Donald Ngoma katika dakika ya 17 akimalizia kazi nzuri ya  Juma Abdul ambaye baadae aliumia na kutolewa nje, nafasi yake ikichukuliwa na Pato Ngonyani.

Kwa ushindi huo Yanga ni kama vile imejisafishia njia kuelekea hatua ya pili ya ligi ya mabingwa Afrika kwani katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo jijini Dar es Salaam, itahitaji japo sare tu ili kusonga mbele.

Yanga sasa imejiweka sawa kisaikolojia kuelekea mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya vinara wa ligi hiyo Simba, ambao utachezwa jumamosi  februari 20 katika dimba la taifa jijini Dar.

Post a Comment

 
Top