BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim BoimandaKIKOSI cha APR ya Rwanda kinatua jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga katika michuano ya klabu bingwa Afrika utakaopigwa kwenye dimba la taifa siku ya jumamosi.

Wanajeshi hao ambao katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali waliadhibiwa mabao 2-1 na Yanga, watatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) majira ya saa 10 alasiri kwa ndege ya shirika la  ndege la Rwandair.

Chanzo chetu cha habari kilichopo  jijini Kigali kilisema  APR itaendelea kuwakosa beki wake wa kushoto Ngabo Albert na mshambuliaji Ndahinduka Michael ambao hawakuwepo kwenye mchezo wa awali kutokana na majeruhi.


Kama ilivyokuwa kwa Yanga, APR nao hawakupangiwa mchezo wowote wa ligi kuu katikati ya wiki hii hivyo kuwa na wakati mzuri zaidi wa kujiandaa na mchezo wa marudiano. 

APR wana wakati mgumu sana kuiondoa Yanga ambayo ilionyesha uwezo mkubwa na kushinda mchezo wa awali. Ili kusonga mbele APR watalazimika kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 na kuendelea.

Post a Comment

 
Top