BOIPLUS SPORTS BLOG

Aubemeyang kulia akiwa na Mbwana Samatta walipokutana Abuja, Nigeria kwenye tuzo za Afrika

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund raia wa Gabon, Pierre Emerick Aubemeyang amesisitiza kuwa hana mpango wa kuihama klabu hiyo msimu ujao.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 32 katika michuano yote hadi sasa amekuwa akizivutia klabu kubwa barani Ulaya zikiwemo Real Madrid, Manchester united, Chelsea na Arsenal huku mwenye kisu kikali ndiye atafanikiwa kumpata mfungaji huyo ambaye ni mchezaji bora wa Afrika.

Katika dirisha la usajili la mwezi January mchezaji huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na klabu kubwa nchini Uingereza lakini zilishindwa kumpata katika dakika za mwisho.

Hata hivyo itakuwa ngumu kwa kocha wa Dortmund Thomas Tuchel kumuachia mshambuliaji ambaye ametengeneza maelewano mazuri na wachezaji Marco Reus, Henrick Mihkytarian huku wakiwa na pointi 64 pungufu ya pointi tano tu dhidi ya vinara Bayern Munich wanaoongoza kwa pointi 69.

Post a Comment

 
Top