BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi WetuTIMU ya Azam Fc leo imejitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye kombe la shirikisho baada ya kuibanjua Bidvest Wits ya Afrika ya kusini mabao 3-0

Azam ilionyesha kuwa imepania kupata ushindi tangu dakika za mwanzo baada ya kufanya shambuli kali katika dakika ya tatu tu ya mchezo ingawa pasi ya mwisho ya Abubakary Salum 'Sure Boy' ilinaswa na mabeki wa Bidvest.

Azam walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya  51 lililofungwa na Sure Boy kwa shuti kali akimalizia mpira uliookolewa na mabeki wa Bidvest kufuatia kona ya Ramadhan Singano 'Messi'.


Makosa ya mabeki wa Bidvest kuzembea kuokoa mpira yaliwagharimu baada ya Shomari Kapombe kuserereka na kuutumbukiza nyavuni katika dakika 56 kabla John Bocco 'Adebayor' kushindilia msumari wa tatu kwenye dakika ya 59.

Azam sasa katika mchezo wa marudiano itahitaji sare au ushindi wowote ili isonge mbele. Kama itapoteza basi iwe kwa magoli yasiyozidi mawili.

Post a Comment

 
Top