BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Zainabu Rajabu, Dar


NAHODHA wa Azam FC, John Bocco aliifunga Yanga  bao moja wiki iliyopita kati ya mabao mawili waliyoshinda kwenye sare ya mabao 2-2 lakini amesema kuwa si kazi rahisi kuwafunga Yanga mfululizo kwani ni timu kubwa na nzuri.

Bocco aliiambia BOIPLUS kuwa ushindi walioupata kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ni kwa sababu walijipanga kupambana kupata matokeo hayo na si vinginevyo.

"Si kazi rahisi, isipokuwa mimi
nimekuwa nikijipanga sana kabla ya mechi na Yanga kwasababu najua hata wao huwa wanajipanga kwa ajili yangu. Huwa nawasoma sana
mabeki wao, makosa yao nayajua na mimi nikiingia uwanjani najua hata wanikabe vipi, lakini kuna wakati wataniachia mwanya nitafanya yangu," alisema Bocco

Bocco ambaye amefikisha mabao 10, alisema kuwa hakuna ubishi kwa sasa kwamba Yanga ndiyo wapinzani wao wakuu kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na timu hizo zote mbili kuwa na vikosi bora.

Azam inasafiri kesho Jumatano  kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya  Bidvest Wits
unaotarajiwa kufanyika Machi 12,  kwenye Uwanja wa Bidvest uliopo jijini  Johannesburg.

Azam watacheza mechi ya marudiano Machi 20, jijini Dar es Salaam ambapo timu itakayofuzu itacheza na mshindi kati ya Esperance ya Tunisia au New Star ya Douala, Cameroon.

Post a Comment

 
Top