BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda

KIPA wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' ambaye alikuwa akiichezea klabu ya IBV Vestmanaeyjar FC ya nchini Iceland, amefariki dunia mchana wa leo kwa ugonjwa wa kansa ya tumbo, mtandao wa KAWOWO.COM umeripoti.

Dhaira aliyekuwa na miaka 28 aligundulika kuwa na kansa ya tumbo mwezi januari mwaka huu nchini Iceland ambako alikuwa akimalizia mkataba wake na IBV

Dhaira alianzia soka lake na Walukuba FC ya Jinja kabla hajahamia Express halafu akaenda URA na baadae kutua Tanzania katika mitaa ya Kariakoo kwenye klabu ya Simba ambako alipoondoka ndipo akaenda Iceland.

Dhaira ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa Cranes, Bright Dhaira  aliyekuwa akiichezea KCCA,  alifanikiwa kunyakua mataji matatu ya CECAFA akiwa na Cranes.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda Uganda kwa mazishi inafanywa na familia yake.

R.I.P ABEL DHAIRA

Post a Comment

 
Top