BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu, D'jamena


NAHODHA mpya wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'  anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta leo amefanya kile ambacho watanzania walikuwa wanakitaka kwa kuifungia timu hiyo bao moja katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 dhidi ya Chad.

Mchezo huo wa kukata na shoka uliopigwa kwenye dimba la Omnisports  Idriss Mahamat Ouya jijini D'jamena ulianza kwa kasi huku kila timu ikionyesha kutafuta bao la mapema ili kutuliza 'pressure' ya mchezo.

Baada ya mashambulizi kadhaa, Samatta aliyekuwa wa kwanza kuwasili kambini nchini humo akitokea Ubelgiji aliifungia Stars bao safi katika dakika ya 30 na ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo akimalizia kwa shuti kali pasi ya Farid Mussa.

Kwa matokeo hayo Stars inayorejea nchini kesho inakuwa imejizolea pointi nne kwenye kundi G baada ya kucheza michezo mitatu ambapo walitoka sare na Nigeria na walipoteza kwa Misri. 

Post a Comment

 
Top