BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
CHAMA cha soka nchini Chad FTFA kimetuma barua kwa CAF na TFF kuelezea kushindwa kwao kusafiri kuja nchini Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sababu ya kushindwa kwao kusafiri kama ilivyoelezwa kwenye barua hiyo ni nchi hiyo kuathiriwa na mgogoro wa kiuchumi.

Hii hapa ni tafsiri fupi ya barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kifaransa.

"TAARIFA YA CHAD KWA CAF NA TFF

Timu yetu haiwezi kusafiri hadi Dar kwa mechi ya tarehe 28
Nchi yetu imeathirika na mgogoro wa uchumi duniani...hivyo ushiriki wetu kwenye mashindano mbalimbali umepata pigo kubwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Tunaomba radhi kwa usumbufu huu ambao ni nje ya uwezo wetu na nia yetu"

Post a Comment

 
Top